×

England Vs Sweeden: Beckham, Zlatan Wawekeana Dau

UBISHI wa kimichezo wa kuwekeana dau umezuka  baina ya nyota wa soka wa Uingereza (England), David Beckham (aliyestaafu) na  Zlatan Ibrahimovic wa Sweden anayeendelea kukipiga.

Malumbano yao yanahusu mpambano wa leo wa Kombe la Dunia baina ya nchi hizo mbili ambao utafanyika leo nchini Urusi.  Beckham amemwambia Ibrahimovic atamnunulia  samani (fanicha) kutoka  kampuni maarufu nchini mwake (Sweden) kwa kuuza zana hizo ambayo inaitwa Ikea

 

Vilevile, Ibrahimovic amemwambia Beckham ajitayarishe kumnunulia chakula cha jioni popote duniani iwapo timu yake ya Sweden itawashinda ‘Simba Watatu’ (England) leo.

Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii, Beckham  amekubali ubashiri huo lakini amesisitiza  Ibrahimovic lazima ahudhurie mchezo wa soka utakaopigwa katika uwanja wa Wembley (England) akiwa amevaa jezi la timu ya Uingereza iwapo timu hiyo inayoongozwa na Gareth Southgate itashinda.

Beckham ni mchezaji wa zamani wa timu ya  LA Galaxy ya Marekani ambayo  Ibrahimovic amejiunga nayo mwezi Machi mwaka huu.

Hivi ndivyo ‘viapo’ vya nyota hao wa soka walivyoweka katika mtandao

Wawili hao  waliwahi kuchezea timu za Paris St-Germain (PSG), Manchester United, AC Milan na LA Galaxy ya Marekani ambako Ibrahimovic (36) yupo sasa.

Raia huyo wa Sweden, alipumzika kucheza soka la kimataifa baada ya mashindano ya Euro 2016, hata hivyo kumekuwa na tetesi huenda akarejea katika soka la kawaida nchini Russia mwaka huu.

Pia amewashambulia viongozi wa soka nchini mwake kwa kumwacha katika simu ya taifa katika michuani ya Kombe la Dunia.

 

England inapigania kufika katika michuano ya nusu-fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990 itakapokutana na Sweden katika dimba la Samara leo.