
MAANDALIZI ya Jukwaa ambapo mwili wa mtoto wa Msanii Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’, Patrick utakapoagwa baadaye leo yamekamilika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwili wa mtoto Patrick aliyeaga dunia Jumanne usiku, Julai 3, 2018 nchini Kenya alikokuwa kitibiwa uliwasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar na kuhifadhwa katika Hospitali ya Agha Khan.

Mwili wake utaagwa leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kuzikwa jioni katika makaburi ya Kinondoni.

Ratiba hiyo ni ifuatayo:
Jumamosi, Julai, 7, 2018.
Saa 2 Asubuhi, kuchukua mwili Aga Khan Hospital.
Saa 3 Asubuhi, familia kuaga mwili nyumbani Mwananyamala.
Saa 5 Asubuhi, Misa ya Kuaga Mwili, Viwanja vya Leaders.
Saa 9 Mchana, Ibada ya Maziko Makaburi ya Kinondoni

Global Publishers na Global TV Online tutakuwa LIVE kukuletea kila kinachojiri kuhusiana na msiba huo.

Mwili tayari umeshafikishwa nyumbani kwa baba wa Marehemu, Mwananyamala jijini dar baada ya kutolewa hospitali.
