The House of Favourite Newspapers

NISHA AKIPIGWA DENDA BABU WA KIZUNGU – VIDEO

STAA wa filamu na muziki Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa kwa sasa amebadili mtazamo na kuamua kuwa na mpenzi anayemzidi umri ‘Babu’ baada ya kukumbuka na sekeseke la kuibiwa mabwana ambao amekuwa nao kwenye mahusiano  ya mapenzi kipindi cha nyuma.

 

Nisha kupitia ukurasa wake wa Instagram amebainisha anapendana na babu huyo huku na kulalamikia kwamba amekuwa mhanga wa mapenzi kwa muda mrefu, kunyang’wanywa mawbana, kusalitiwa na kudai kuwa akitembea na vijana wadogo anaambulia matusi.

 

“Ni ngumu sana kuficha hisia zangu kwa mtu nnayempenda, nimeshakuwa na m-black, Mwarabu ila kote niliambulia usaliti na uongo wa mapenzi, niliwahi sikia Wazungu wana mapenzi ya kweli kuliko Waafrica, kujaribu si mbaya.

 

“Me ni msafiri sijafika bado, na Mwenyezi Mungu anajua kama hapa ndo mwisho wa safari yangu au inaendelea, kikubwa nimeshampata na maneno sijali,’ amesema Nisha.

 

Katika post nyingine Nisha amesema;

“Walimwengu sijui mna nini, nikiibiwa bwana mnanyamaza kimya, nikiwa na wa rika langu ben 10, akinizidi umri kizee, au mlikuwa mnafurahia kujiita bachelor? Sasa nimeshampata bado maneno kedekede. Yeye na mimi kwani tuna kasoro gani? Au mimi nimezaliwa niliye tu na kuibiwa?” amehoji Nisha.

Hivi karibuni nisha alisema amekuwa akiteswa na mapenzi la wanaume wenye umri mdogo ‘kibenteni’ kutokana na kumgeuza ‘ATM’ kwa kumuhudumia kama mwanaye.

 

Nisha ameachia video mtandaoni ikimwonyesha akipigwa denda na babu huyo wa Kizungu huku akizungumza kauli za kumvutia kumahaba.

Comments are closed.