×

Airtel Yatangaza Washindi wa Amsha Amsha

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza jambo.
Meneja Masoko wa SportPesa, Sabrina Msuya akifafanua jambo.

 

 

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na SportPesa imetangaza washindi wa wiki ya tatu ya promosheni ya mwezi mmoja ya Amsha Amsha na Airtel Money na ushinde ambayo ilizinduliwa Juni 14, mwaka huu.

 

 

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema droo ya kupata washindi hao imesimamiwa na kuchezeshwa kwa uwazi na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ambao ndiyo wenye jukumu la kusimamia michezo yote ya bahati nasibu.

“Leo washindi  kumi wamejishindia simu mpya za ‘smartphone’ kila mmoja, wengine kumi wamejihakikishia tiketi ya kushuhudia mechi za Simba na Yanga kwa msimu ujao wa 2018/2019, hivyo natoa rai kwa wateja wote kushiriki kwenye promosheni hii ya Amsha Amsha na ushinde na Airtel Money,” alisema Mmbando na  kuongeza kuwa mshindi mmoja wa siku atajishindia TV mpya ya inchi 32 na ving’amuzi kutoka Star Times.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa SportPesa, Sabrina Msuya amewataka wateja wao kuendelea kubet kwa kutumia Airtel kupitia promosheni hiyo inayoendelea ambayo inaingia hatua ya nne ili wajishindie zawadi zao.