×

Ukraine Yapata Eneo Lililozikwa Watu Wengi Huko Izyum Baada ya Warusi Kutimuliwa

Eneo lililozikwa watu wengi Izyum

ENEO lililo beba miili zaidiya mianne arobaini (440) lilipatikana huko Izyum kaskazini mashsriki mwa Ukraine, ambako vikosi vva Urusi vilifukuzwa siku chache zilizopita katika eneo hilo taarifa hiyo ilitolewa na maafisa wa Ukraine alhamisi.

 

Serhiy Bolvinov mpelelezi mkuu wa polisi wa mkoa wa Kharkiv aliiambia Sky News kwamba “Naweza kusema ni moja ya maeneo makubwa zaidi ya mazishi katika mji mkubwa katika maeneo yaliyokombolewa, miili 440 ilizikwa katika sehemu moja”. Akasema pia katika miili hiyo “Wengine walikufa kwa sababu ya moto wa mizinga, wengine walikufa kwa sababu ya mashambulizi ya anga.”

Eneo lililozikwa watu wengi Izyum

Mashambulizi ya Ukraine yaliwasukuma wanajeshi wa Urusi kutoka eneo hilo wikendi iliyopita, Warusi walikuwa wakiukalia mji katika mkoa wa Kharkiv. Maafisa wa Ukraine walisema wanajeshi hao waliacha nyuma kiasi kikubwa cha risasi na vifaa.

 

Volodymyr Zelenskyy Rais wa Ukraine ambaye alikuwa ametembelea mji huo uliotekwa tena hivi majuzi siku ya Jumatano, alisema Warusi walihusika. Alifananisha ugunduzi huo huko Izium na tukio kama hilo huko Bucha, kitongoji cha Kyiv wakati wa hatua za mwanzo za uvamizi wa Urusi mwishoni mwa Februari.

 

Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment