The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Kujua Wabaya Wao Le

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), leo Jumatano linatarajiwa kutoa ratiba ya msimu wa 2018/19 wa Ligi Kuu Bara ambapo ligi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi ujao.

 

Ratiba hiyo itakuwa na idadi ya timu 20 kutoka 16 za msimu uliopita ambapo ndipo timu kongwe za Simba na Yanga zitaweza kuwafahamu wabaya wao watakaopambana nao msimu mzima wa 2018/19.

 

Wakati ratiba ikitarajiwa kutolewa leo, kumekuwa na utata wa mdhamini wa ligi hiyo kwa msimu uliopita, Kampuni ya Vodacom kama ataendelea kuidhamini ligi hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

 

Kutokana na hali hiyo, TFF imesema kuwa, hilo litatolewa ufafanuzi leo wakati wa kuitangaza ratiba hiyo ili kuondoa wasiwasi uliopo.

 

Bado Vodacom wana nafasi ya kuendelea kuwa wadhamini wa ligi hiyo kwa kuwa baada ya mkataba kumalizika, walikaa na TFF kufanya majadiliano ya mkataba mpya.

Comments are closed.