×

MIKE AMRUHUSU THEA KUOLEWA

Tokeo la picha la MIKE SANGU
Michael Sangu ‘Mike’

BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu, Ndum­bagwe Misayo ‘Thea’ kufunguka kuwa ana mpango wa kubeba mimba ya mwanaume mwingine ili ndoa yake ya kanisani ivunjike rasmi, aliyekuwa mume wake ki­sha wakatengana, Michael Sangu ‘Mike’ ameibuka na kumpa ruhusa mwanama­ma huyo kuolewa au kuzaa hata na wanaume kumi.

 

Mike aliiambia Za Motomoto News kuwa, Thea ana uhuru hata wa kuolewa au kuzaa na mwa­naume yeyote anayemtaka kwani yuko huru hakuna sheria yoyote inayo­mbana kwa kuwa wakati wanafunga ndoa katika Kanisa Katoliki, walifunga ya mseto hivyo muigizaji huyo akawa anaendelea kusali kwenye kanisa la kilokole alikokuwa tangu mwanzo.Tokeo la picha la Ndum­bagwe Misayo ‘Thea

 

“Thea yuko huru kuolewa au kuzaa hata na wanaume kumi maana hakuna kinachomzuia, shida iko kwangu maana dini ya Katoliki inatambua ndoa moja tu ambayo nili­funga naye na hatujawahi kuibatilisha,” alisema Mike ambaye pia ni msanii wa filamu Bong

Stori : Mwandishi wetu.