
KWA masikitko makubwa, uongozi wa Makampuni ya Global Group unasikitika kutangaza kifo cha mama mzazi wa Mkurugenzi wao Eric James Shigongo, Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia alfajiri ya leo Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akitibiwa.
Akitangaza msiba huo, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho amesema msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu zote za msiba zitafanyika.

Kwa niaba ya wafanyakazi wa Makampuni ya Global Group, tunapenda kutoa pole kwa familia ya Shigongo, pole kwa ndugu jamaa na marafiki, pole kwa wafanyakazi wenzetu kwa kupata pigo la kuondokewa na mpendwa wetu.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe, AMEN!