



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na ujumbe wa Wanafunzi, Walimu na Wafanyakazi wa Chuo cha Teknolojia Cha Dar es Salaam (DIT) walio kwenye ziara Katika Halmashauri ya Chalinze. Wakiwa katika ziara hiyo walipotembelea Shule ya Sekondari ya Kiwangwa na kuzungumza na Wanafunzi na kuwapa pole kwa ajali ya Moto uliyounguza Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo.
Wakiwa shuleni hapo wameona pia ujenzi wa Bweni Jipya ambalo linaanza kujengwa ambalo likikamilika wanafunzi wataza kulitumia, pia wamegawa masweta, na kuwapa moyo wa kusoma sayansi licha ya kadhia hiyo iliyowakumba.#KaziIendelee.