WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric James Shigongo, marehemu Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia leo kwa ajili ya kutoa pole kwa wanafamilia kwa kuondokewa na mama yao.
Bi. Kapela amefariki dunia alfajiri ya leo Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ambapo msiba huo upo nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu zote za mazishi zitafanyika.
Mwili wa marehemu Asteria Kapela unatarajiwa kuagwa Jumatatu na kusafirishwa kwenda nyumbani Mwanza na mazishi yatakayofanyika Jumatano ijayo.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe, AMEN!
Comments are closed.