×

Waziri Mwakyembe Atembelea Studio Za Global TV Online

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mbele) akimuongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwenda studio za Global TV Online alipofika katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam leo.
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa na wafanyakazi wa Global Group ndani ya studio ya Global TV.
Kiongozi wa Global TV Online, James Range (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Mwakyembe.
…Waziri Mwakyembe akijionea matayarisho ya vipindi vya Global TV.
Mtangazaji wa Global TV Online na Muhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kulia) akifanya mahojiano na Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe akiendelea kufafanua jambo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe leo ametembelea Kampuni ya Global Group ambayo ndani yake kuna Global TV Online ambapo alipata fursa ya kutembelea studio zza Global TV.

katika ziara hiyo Waziri Mwakyembe ampata maelezo ya namna ambavyo Global Tv Online inavyoweza kutumia teknolojia ya Kubalisha Background ya kijani na matumizi ya Vitual Studio katika kurusha matangazo yake.

Mkuu wa Idara ya Global Tv James Range amemuelezea Waziri Mwakyembe kuwa kwa kutumia Green Screen Technology wanaweza kubadili muonekano wa studio na kuwa wa kisasa zaidi kadiri ya mahitaji ya vipindi husika.

Akiwa katika Studio za Global Tv, Waziri Mwakyembe ameweza kufanyiwa mahojiano maalumu na Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli ambapo Mh Waziri amepata fursa ya kufafanua masuala kadhaa ya kitaifa