×

MSHINDI WA PIKIPIKI APATA MCHECHETO, ASAHAU NAMBA YAKE YA SIMU


Mambo ni motooo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mchecheto wa ushindi alioupata Ramadhan Mohamed baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa pikipiki mpyaaa katika Droo ya Kumi ya Shindano la Tusua Maisha na Global, iliyochezeshwa Jumanne ya Agosti 28, na kurushwa mubashara na Kituo cha Runinga cha Global TV.

 

Katika droo hiyo, Ramadhan Mohamed, mkazi wa Morogoro ambaye kwa sasa yupo Zanzibar kikazi, alitangazwa kuwa mshindi wa pikipiki lakini katika hali ya kushangaza, mshindi huyo alipotakiwa kutaja namba yake ya simu, aliisahau kwa muda kutokana na furaha ya ushindi.

 

Iliwalazimu waendeshaji wa droo hiyo, kumpa dakika kadhaa mshindi huyo ambaye ni mfanyakazi katika kiwanda kimoja visiwani Zanzibar, atulize nafsi yake kwanza kutokana na kuzidiwa na mchecheto wa ushindi, ndipo alipofanikiwa kuikumbuka, huku akiwa haamini kabisa kwamba kweli ameshinda zawadi hiyo.

 

Wengine waliong’ara katika droo hiyo ni Geofrey John mkazi wa Chanika aliyejishindia dinner set na ?Justice Rugambwa mkazi wa Gongolamboto aliyejishindia zawadi ya jezi.

 

“Washindi hawa wa droo ya kumi wataungana na wenzao waliong’ara katika droo ya tisa ambao ni Ramadhan Simba, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam aliyejishindia pikipiki, Anna Mbise wa Arusha aliyejishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro aliejishindia jezi na tunatarajia kuwakabidhi zawadi zao wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa kampuni ya Global Publishers.

 

Ili kuwa miongoni mwa washindi, unachotakiwa ni kununua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra.

 

Ukishanunua, funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

 

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi vigezo na masharti vinazingatiwa.