×

MBOTO: NINGEMUOA RIYAMA NINGEPATA TABU SANA !

rimaya444
Haji Salum ‘Mboto’ na Riyama Ally

MSANII wa filamu za Kibongo, Haji Salum ‘Mboto’ amesema endapo angemuoa msanii mwenzake Riyama Ally ambaye wamekuwa wakinoga sana kwenye filamu za vichekesho, angepata tabu sana.

Mboto alisema hayo hivi karibuni baada ya kunaswa na Riyama ndani ya kiwanja cha burudani cha City Garden kilichopo Railway Gerezani jijini Dar ambapo walikuwa wakiandaa tamthiliya.

“Yaani Riyama angekuwa mke wangu nahisi ningepata tabu sana, kwa hivi vituko vyake anaonekana angenipelekesha sana hata katika maisha ya kawaida.”

Stori: Richard Bukos, Amani.