Mwanafunzi wa Dhule ya Sekondari ya Kalangalala mkoani Geita, Jonathan Mkono aliyepigwa na mwalimu wake na kulazwa hospitalini, ameruhusiwa kutoka hospitali leo mchana Septemba Mosi, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Geita, Dk. Moses Simon amesema mwanafunzi huyo ameruhusiwa baada ya afya yake kuimarika.

Amesema alifikishwa hospitalini hapo akiwa na maumivu baada ya kuchapwa fimbo mgongoni na kwamba hakuna eneo ambalo amevunjika.
Mwanafunzi huyo hakuweza kueleza hali yake kwa sasa baada ya walimu kumchukua na kumzuia kuzungumza na waandishi wa habari.