




Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo ametembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara zinazojengwa katika jiji lake na kuridhishwa na ujenzi huo inayojengwa chini ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADs) inayogharimu zaidi ya Bilioni 24.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo, Makonda, amesema hatua iliyofikiwa inaridhisha.

Katika ziara hiyo Makonda amekagua barabara ya Wazo hadi Mbenzi Luis, Goba hadi Mbezi Masana ambapo ujenzi wake ni wa kiwango cha lami.
Aidha Makonda amesema ujenzi wa daraja la kivuko cha watembea kwa miguu katika barabara ya Bagamoyo eneo la Lugalo uko katika hatua za mwisho na umegharimu zaidi ya Bilioni 1.
Makonda amesema, kukamilika kwa barabara hizo kutafungua fursa kwa wananchi na kuwezesha maendeleo katika maeneo hayo. Pia ameeleza kuwa huo ni utekelezaji wa ahadi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli.