
Mbunge wa Serengeti, Mwita Rioba amemwambia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kuachia nafasi yake ya Ubunge kama itawezekana ili kufanikisha ujenzi wa Barabara inayounganisha Mkoa wa Mara na Mkoa wa Arusha.
Akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mbuzi Mjini Mugumu Mbunge huyo wa CHADEMA amesema, yupo tayari kuachia Ubunge huo ikiwa Barabara hizo zitajengwa na kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi.