
HIKI ni ‘kipigo cha mbwa koko’! hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya mabingwa wa pili wa kombve la Dunia, Croatia chini ya staa wao, Luka Modric kuambulia kipigo cha aina yake usiku wa kuamkia leo na timu ya Taifa ya Hispania.

Dakika 35 tu za kipindi cha kwanza zilitosha kuona aibu inayokuja kwa timu ya taifa ya Croatia katika mchezo huo kwenye michuano ya UEFA Nations League ambapo tayari Saul Niguez, Marco Asensio na bao la kujifunga la Lovre Kalinic yaliufanya mchezo kwenda half time kwa Hispania kuongoza kwa mabao 3-0.

Croatia walirudi kipindi cha pili wakiwa na juhudi ya kutafuta kuchomoa lakini tabu ikawa pale pale baada ya kufungwa 3 zingine na kuwa 6 huku safari hii wafungaji wakiwa Rodrigo, Sergio Ramos na Isco.

Hiki ndio kipigo kikubwa zaidi kwa Croatia kuwahi kukipokea na wengi wameshangazwa kwa namna walivyotepeta hii leo haswa ukizingatia kwamba hawa ni washindi wawili wa michuano ya kombe la dunia.

Spain (4-3-3): De Gea 6; Carvajal 8 (Azpilicueta 75), Nacho 6, Ramos 7, Gaya 6; Ceballos 7, Busquets 6 (Rodri (59), Saul 7 (Alcantara 65); Asensio 9, Rodrigo 8, Isco 6

Goals: Saul 24, Asensio 33 Kalinic OG 35, Rodrigo 49, Ramos 57, Isco 70

Croatia (4-2-3-1): Kalinic 6; Vrsalijko 7 (Rog 20), Mitrovic 6, Vida 6, Pivaric 6; Rakitic 6, Brozovic 6 (Pjaca 62); Kovacic 6, Modric 6, Perisic 6; Santini 5 (Livaja 71)
Booked: Santini, Brozovic