The House of Favourite Newspapers

YANGA YASHINDA DHIDI YA STAND UNITED, BAO 4-3

Timu ya Yanga wamepata ushindi wa mabao 4-3 kutoka kwa Stand United ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Yanga inafikisha pointi sita katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu, zote ikishinda kwa tofauti ya bao moja, baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 2-1 katika mchezo wake wa kwanza, wakati Stand United inabaki na pointi zake sita baada ya mechi nne.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Benedict Magai aliyesaidiwa na Michael Mkongwa na Mashaka Mwandembwa, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-1.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; Klaus Kindoki, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kevin Yondan/Abdallah Shaibu ‘Ninja’ dk80, Feisal Salum, Mrisho Ngassa/Yussuf Mhilu dk62, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo, Ibrahim Ajib/Raphael Daudi dk62 na Deus Kaseke.

Stand United; Mohammed Makaka, Bigirimana Ramadhani, Ndoriyabija Eric, Erick Mulilo, Niyonkuru Nassor, Erick Mbirizi, Datius Peter/Charles Chinongo dk55, Jackob Massawe, Alex Kitenge, Hafidh Mussa na Sixtus Sabilo.

Comments are closed.