The House of Favourite Newspapers

TUNDA AMFUNGUKIA ALIYEDAIWA BWANA’KE

Image result for tunda na casto dickson
Tunda Sebastian

BAADA ya picha akiwa anazu-ngumza na mwanaume kwenye Mtandao wa Snapchat kusambaa mitandaoni na kudaiwa kuwa ndiye bwana’ke mpya, video queen maarufu Bongo, Tunda Sebastian ameibuka na kufungukia madai hayo. Akipiga stori na Risasi Vibes, Tunda ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Casto Dickson alisema mwanaume huyo aliyekuwa anachati naye ni rafiki yake wa kawaida tu na siyo mpenzi wake kama watu wanavyodai.

“Jamani nawashangaa sana watu maana siyo kila ninayeongea naye ni mpenzi wangu, huyu ni rafiki yangu tu wa kawaida hivyo nawasihi watu wasiwe na tafsiri za mapenzi tu kila wakati,” alisema Tunda.

RISASI VIBES

Comments are closed.