×

NANDY APATA MPENZI MWINGINE

Image result for Faustine Charles ‘Nandy’
Faustine Charles ‘Nandy’

MSANII wa Bongo Fleva ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya Aibu, Faustine Charles ‘Nandy’ amefunguka kwamba kwa sasa hana ukaribu wa aina yoyote ile na msanii mwenzake, William Lyimo ‘Billnas’ ambaye pia amewahi kuwa mpenzi wake, baada ya matatizo yaliyowahi kutokea ya kuvuja kwa video yao chafu.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Nandy alisema kwa sasa hivi ameopata mpenzi mwingine na kama Mungu akijalia, hivi karibuni atafunga ndoa. Nandy amezungumza mengi, ungana naye hapa chini;

Risasi Vibes: Kwa nini kipindi hiki uliamua kuja na wazo la Wimbo wa Aibu na siyo kitu kingine?

Nandy: Ni kwa sababu ya mashairi na jinsi mambo yalivyokuwa yanasambaa mitandaoni, kwa hiyo tukaona Aibu ndiyo itapendezea ‘ku-cover’ kwenye huo wimbo.

 

Risasi Vibes: Vipi kuhusu video?

Nandy: Video itatoka hivi karibuni, japo siwezi kusema ni lini, ila watu wawe tayari tu wataiona.

Risasi Vibes: Mashabiki wameupokeaje wimbo wako wa Aibu?

Nandy: Namshukuru Mungu Aibu imepokelewa vizuri sana, nahisi pia sababu ni muziki ambao nimejaribu kuimba ladha tofauti.

 

Risasi Vibes: Kuna huu mfumo wa wasanii kutoa nyimbo kwa siku moja, mfano hivi karibuni umetoa wewe wimbo wako huo kisha Maua Sama naye akatoa Iokote, vipi kwa upande wako haishushi thamani ya wimbo wako wala kukuathiri?

Nandy: Hapana, kwa upande wangu mimi hainiathiri kitu chochote kwa sababu kila mtu ana nafasi yake, kila mtu ana mashabiki wake na ninavyofahamu ni kwamba shabiki hawezi kusikiliza wimbo mmoja tu kila siku, lazima atataka kusikiliza, Maua kafanyaje, Nandy kafanyaje, ladha tofautitofauti kwa hiyo haiwezi kushusha thamani ya wimbo wangu.

 

Risasi Vibes: Kuna kipindi uliwahi kuongea kwamba unatamani kufanya kolabo na Ruby, vipi bado una huo mpango?

Nandy: (Anaguna) bado kidogo (anacheka) bado kiukweli, nafikiri management (uongozi) yangu na yake zikifikia muafaka tutafanya.

Risasi Vibes: Vipi lakini unatamani iwe hivyo?

 

Nandy: Yah ni kazi, ikitokea tutafanya.

Risasi Vibes: Uhusiano wako na Ruby kwa sasa hivi ukoje?

Nandy: Hatuna uhusiano wowote, kwa sababu sisi siyo marafiki, hatujazoeana kwa hiyo tupo tu kawaida, najua yupo na yeye anajua nipo basi.Related image

Risasi Vibes: Ilikuwaje mpaka ukapata shavu la ubalozi kwenye kampuni ya simu (jina linahifadhiwa)?

Nandy: Kiukweli naishukuru sana management yangu kwa kusimamia vyema ‘brandi’ yangu na nyingine ambazo napata, ni kitu kikubwa sana ambacho nimekipata kwa mwaka huu, shavu hili la kampuni ya simu limenibadilisha sana maisha yangu.

Risasi Vibes: Ni vigezo gani ambavyo huwa wanaviangalia kabla ya kukupa kazi?

 

Nandy: Sijui kiukweli kwa sababu nilikwenda nikasaini mkataba, nikapewa kazi na nikaifanya, kwa hiyo wao ndiyo wanajua ni vigezo gani ambavyo wanaviangalia.

Risasi Vibes: Ulijisikiaje baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wao?

Nandy: Nilijisikia vizuri, unajua msanii kupata mkataba, tena kwa kipindi hiki ambacho watu wanalalamika hawana pesa ni kitu kikubwa sana, kwa hiyo nilijisikia vizuri sana kuona kwamba kumbe brandi inaonekana na uzito wangu unaonekana.

 

Risasi Vibes: Umesaini mkataba wa kiasi gani?

Nandy: Siwezi kusema kabisa kuwa nimesaini mkataba wa kiasi gani ila ni kuanzia shilingi milioni 70 na kwenda juu.

Risasi Vibes: Ni mkataba wa muda gani?

Nandy: Mkataba wa mwezi mmoja na nusu.

Risasi Vibes: Ulisema kwamba mwaka 2020, utaacha kufanya muziki, sababu kubwa ni nini?

 

Nandy: Siyo kwamba nitaacha kabisa kufanya muziki ila nitapunguza shughuli za muziki, nitafanya biashara, hapa nilipo kuna vitu ambavyo tunavitengeneza kama brandi ya Nandy kwa ajili ya baadaye na ndoto yangu kubwa ni kufanya biashara na nafikiri nipo vizuri sana kwa hilo.

Risasi Vibes: Unazungumziaje wimbo wa Madam Hero wa Hamisa Mobeto?

Nandy: Muziki ni ubunifu na kila kitu kinaanza taratibu, kwa hiyo kama akifanya vizuri na akakaza, namuona mbali kwa kweli.

 

Risasi Vibes: Tangu lile tatizo lako na Billnas litokee, hujasikika tena na mwanaume mwingine, vipi upo kwenye uhusiano au ndiyo ulishakata tamaa?

Nandy: (Anacheka) hapana shemeji yenu yupo, tusubiri ndoa tu kama Mungu akijalia.

Risasi Vibes: Ndoa itakuwa lini?

Nandy: Siwezi kutaja ni lini kwa sababu naweza nikataja halafu isifanyike, kwa hiyo sasa hivi namuomba tu Mungu iweze kutimia.

 

Risasi Vibes: Uhusiano wako na Billnas sasa hivi ukoje? Bado ni washkaji au mliacha kuongea baada ya video yenu chafu kusambaa?

Nandy: Hatuna ushikaji kiukweli tangu kipindi kile tatizo lilipotokea, hatujawahi kuwasiliana hata kwenye simu, ila nakumbuka mara ya mwisho tulionana central kituo cha Polisi, kwa hiyo sidhani kama kuna kitu chochote cha kuongea, japo najua tukikutana lazima tutapiga stori, tutacheka na kufurahi pia.

Risasi Vibes: Unahisi kwa nini wasanii wengi sasa hivi wameamua kujikita sana kwenye biashara au ujasiriamali?

 

Nandy: Naona ni kitu kizuri kwa sababu sanaa peke yake haitoshi, mfano ukiangalia sisi wasanii wa hapa Tanzania tunahangaika sana kufikisha malengo yetu yaende kimataifa na hata yakifika kimataifa bado kuna kuhangaika sana ili uweze kuwa juu kama wengine walivyokuwepo, kwa hiyo usipowahi mapema katika hapa unapopata jina na pesa kidogo kutengeneza urahisi wa plan B kwenye nchi yako itakuwa ni ngumu sana kwa baadaye. Kwa hiyo ndiyo maana nahisi watu wameshaanza kujua mapema nini cha kufanya.

“DIAMOND Nitamvuta Tu, Ndoa ya Lulu Nina Mpango!!” MALIKA