×

KHADIJA YUSUF AMALIZA BIFU NA WIFI YAKE

Image result for khadija yusufu na leila
Khadija Yusuf

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye muziki wa Taarab ambaye ni dada wa mwimbaji maarufu wa muziki huo zamani kabla hajamrudia Mungu wake, Mzee Yusuf, Khadija Yusuf ameweka wazi kuwa amemaliza bifu na wifi yake yaani mke wa kaka yake huyo, Leila Rashidi.

 

Akizungumza na Risasi Vibes katika mahojiano maalum, Khadija alisema yeye na wifi yake walikuwa hawaongei kwa muda wa miaka minne hivyo kulikuwa na bifu zito lakini kwa sasa wameweka mambo sawa, maisha ya maelewano yanaendelea.

Aliendelea kusema kuwa, Mzee Yusuf alipotangaza kuacha muziki, vita kali ya maneno kati yao iliongezeka zaidi, hali iliyosababisha pia Kundi la Jahazi Modern Taarab kusambaratika taratibu ambapo wasanii walioondoka na kila mmoja kwenda kujitegemea kimuziki.

 

Khadija amezungumza mengi, ungana naye hapa chini kwa maswali na majibu;

Risasi Vibes: Ni kwa nini vita iliongezeka baada ya Mzee Yusuf kuacha muziki?

Khadija: Sababu ni kwamba nilitoa wimbo uliokuwa unamlenga wifi yangu Leila ambao ulieleza kuwa yupo mbioni kuachwa na kaka yangu.

Risasi Vibes: Je, uliimba yuko mbioni kuachwa kwa sababu gani?

 

Khadija: Niliimba kwa sababu Mzee Yusuf alimrudia Mungu lakini mkewe Leila akawa anagoma kuacha muziki na kumfuata mumewe kwani sheria za dini ya Kiislam zinataka mume akifanya jambo na mke amfuate.

Risasi Vibes: Lakini kabla ya Mzee Yusuf kuacha muziki wewe na wifi yako mlikuwa hamuongei, ni kwa nini?Image result for khadija yusufu na leila

Khadija: Ni mambo tu ya kifamilia siwezi kuyazungumzia sana kwa kuwa kwa sasa tuko sawa tumemaliza tofauti zetu.

Risasi Vibes: Lakini kuna habari kwamba bifu lenu lilitokana na wewe kuwa ulikuwa unampenda zaidi mke mdogo wa kaka yako ambaye kwa sasa ni marehemu, Chiku Khamis hili likoje?

Khadija: Jamani naomba nisizungumzie hilo kwa sasa maana yameshapita kama nilivyosema.

Risasi Vibes: Ni nani aliyewapatanisha na kumaliza tofauti zenu?

 

Khadija: Kaka yangu Mzee Yusuf ndiye aliyetupatanisha na kuniambia tuyamalize hayo mambo ya bifu za kifamilia hayasaidii na kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu akatupa vifungu vya mwenyezi Mungu anavyotaka, tukayamaliza.

Risasi Vibes: Kwa hiyo kwa sasa wewe na wifi yako mnasalimiana?

Khadija: Ndiyo tunasalimiana, tunatembeleana na tunapendana kwa kweli yale ya zamani yalishapita.

Risasi Vibes: Turudi kwenye muziki, mbona uko kimya kulikoni?

Khadija: Ukimya wangu ulitokana na kutokuwepo hapa nchini kwani nilikuwa Uarabuni ambako nilikuwa nafanya muziki wa taarab asilia.

Risasi Vibes: Ulikuwa Uarabuni nchi gani?

Khadija: Nilikuwa Oman.Related image

Risasi Vibes: Baada ya kutoka huko, umejipangaje kimuziki?

Khadija: Niliporudi nilimtafuta mtunzi Fatma Maulid ambaye alinitungia nyimbo sita.

Risasi Vibes: Kati ya hizo nyimbo sita umeshatoa hata mmoja?

Khadija: Kwa sasa nimetoa wimbo mmoja unaojulikana kwa jina la Unavyotaka Nataka na nyingine mbili nimezirekodi bado kutoa tu.

Risasi Vibes: Utaendelea kuimba peke yako au una mpango wa kuingia kwenye kundi?

Khadija: Nimeamua kutoka mimi kama mimi kwa sababu nina malengo ya kuja kuwa na kundi langu hapo baadaye.

Risasi Vibes: Muziki wa Taarab unaonekana soko lake kupotea, je umejipangaje kuhakikisha unarudi kama zamani?

Khadija: Kwangu soko la taarab bado linalipa ndiyo maana nafanya muziki huu na nimekusudia kuja kivingine na kwa usahihi zaidi na ninaamini nitabadilisha kabisa muziki wa Taarab kutoka ulipo sasa kwenda mbele zaidi hata ya ulivyokuwa zamani.