
LICHA ya mashabiki wengi kudai kwamba anayestahili kuchukua nafasi na kuwa mrithi wa aliyekuwa staa maarufu wa vichekesho Bongo, marehemu Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ni msanii mwenzake, Jacob Stephen ‘JB’, mwenyewe ameibuka na kukataa.
Akipiga stori na Za Motomoto News, JB alisema mashabiki wengi wamekuwa wakimwambia kwamba yeye ndiye mrithi wa Mzee Majuto, lakini haiwezekani kushika nafasi yangu maana alikuwa na ladha yake na yeye ana ladha yake katika uigizaji.
“Haiwezekani mimi kuwa mrithi wa Mzee Majuto maana alikuwa na kitu cha tofauti sana na alipendwa na watu wengi hivyo ni vigumu kuwa mrithi wake ila ninawaahidi Watanzania kuwafurahisha kwa kadiri ya uwezo wangu katika kuigiza,” alisema JB.
STORI: Gladness Mallya, Dar