KAJALA ATEKETEZA MIL 16 MKONONI
STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja amenaswa akiwa ameteketeza fedha nyingi kwenye kununua saa yake ya mkononi ambayo inamchanganyiko wa dhahabu na almasi pamoja na bangili ambazo kwa pamoja vina thamani ya milioni 16.
Akizungumza na Star Showbiz, Kajala alisema kuwa, alinunua saa hiyo na bangili wakati akiwa nchini Dubai na alifanya hivyo kwa sababu aliipenda sana seti hiyo na ni moja ya vitu ambavyo anapenda kuwa navyo.
“Unajua naweza kupenda kitu leo nikawa nachanganyikiwa nacho kabisa maana nilitokea kuvipenda nikasema nikirudi mara ya pili nitanunua maana mara ya kwanza hela yangu haikutosha,” alisema Kajala ambaye anatajwa kuingiza mkwanja mwingi kutokana na ubalozi pamoja na kazi yake ya sanaa.
STORI: IMELDA MTEMA
Comments are closed.