×

ZIDISHENI MATUMIZI YA TEHAMA MAHAKAMANI: JAJI MZUNA

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya Longido, Mhe. Aziza Temu akimuonesha kitu Mhe. Jaji Mfawidhi wakiwa katika jengo la Mahakama la Wilaya Longido linaloendelea kujengwa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ngorongoro,  Mhe. Demetrio Nyakunga  akisoma taarifa ya utendaji wa Mahakama hiyo mbele ya Mhe. Jaji Mfawidhi.
Mhe. Jaji Mzuna akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya mwanzo Namanga.
Mhe. Jaji Mzuna akionyeshwa mipaka ya kiwanja cha Mahakama ya mwanzo Namanga.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido lililopo katika ujenzi.
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha,  Mhe. Mosses Mzuna na Viongozi wa Mahakama, Kanda ya Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya-Ngorongoro

 Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu- Kanda ya Arusha, Mhe. Mosses Mzuna amewakumbusha Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Ngorongoro kuongeza kasi ya matumizi ya TEHAMA.

 

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Mhe. Jaji Mfawidhi alisema kuwa kipindi hiki cha mabadiliko ya Mahakama ya kutumia TEHAMA watumishi wanalazimika kujifunza na kuelewa matumizi hayo ili kuendana na azma iliyokusudiwa.

 

Mhe. Jaji Mzuna alitoa mfano juu ya Mfumo wa kusajili mashauri wa Kieletroniki ujulikanao kama JSDS II kuwa ni muhimu watumishi wote kuufahamu ili waweze kwenda sawa na kasi ya mabadiliko hayo.

Mbali na matumizi ya TEHAMA; Mhe. Jaji Mfawidhi aliongeza kwa kuwaasa Watumishi hao kufanya kazi kwa umoja na bidii ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora zaidi.

 

“Msijihusishe na vitendo vya rushwa kwani vinaharibu Taasisi na pia vitawaharibia maisha yenu, mnachotakiwa kuzingatia ni maadili ya kazi kwa muda wote muwapo eneo la kazi na kutumia lugha nzuri pindi mnapohudumia wateja,” alisisitiza Mhe. Jaji Mzuna.

 

Katika ziara hiyo alipata taarifa ya kiutendaji wa Mahakama hizo kutoka kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mhe. Demetrio Nyakunga.

 

Aidha; Mhe. Jaji Mzuna alipata nafasi ya kutembelea Mahakama ya Mwanzo Waso Loliondo, Mahakama ya Wilaya Longido, Mahakama ya Mwanzo Namanga na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya wilaya ya Longido.

 

Katika ziara yake, Mhe. Jaji Mfawidhi aliambatana na Watendaji wengine wa Mahakama Kanda ya Arusha, lengo likiwa ni kujitambulisha kwa watumishi  na kujua mazingira ya  Mahakama zote zilizopo ndani ya kanda ya Arusha.

Na Catherine Francis, Mahakama  Kuu Arusha

Masaa 3 Lema Kuhojiwa POLISI Kuhusu MO Atoka na Kutema cheche