×

Katavi: Polisi Yazima Ndoa Mwanafunzi Darasa la 5

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi limewakamata watuhumiwa 15 wakiwemo wazazi wawili kwa kumwozesha mwananfunzi wa darasa la tano anayesoma shule ya msingi ya Kaseke iliyopo manispaa ya Mpanda kwa mahari ya ngombe 12.

 

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga, amesema katika mahojiano na watuhumiwa hao jeshi liliweza kugundua mbinu ya udanganyifu waliyoitumia kwa kuwaweka wahusika wawili, Stela Paul (20) na Samsoni Charles (23) kama wanandoa.

 

Kamanda Kuzaga amesema Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuisambaratisha ndoa hiyo ya kimila huku likiendelea na juhudi ya kumtafuta muoaji aliyetoroka.

 

Aidha, Kamanda kuzaga amesema jeshi halitosita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au kikindi cha watu watakaofanya hivyo na hatimaye kuwafikisha mahakamani.

 

Leave a Comment