
MTOTO wa staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifa Nasibu Abdul ‘Tiffah’ amevunja rekodi ya kuwa mtoto wa kwanza kufikisha wafuasi ‘followers’ wengi (zaidi ya milioni 2) katika ukurasa wake wa Instagram kuliko watoto wa mastaa wote Afrika. Mapema wiki iliyopita, Tiffah anayetumia jina la Princess_ tiffah kwenye ukurasa wake wa Insta, alifikisha idadi hiyo ambayo inamfanya kuwafunika watoto wengi wa mastaa ‘Wazungu’. Ijumaa limekuchambulia baadhi ya watoto wa mastaa hao ambao Tiffah amewafunika kwa kufikisha
ASAHD KHALED
Ni mtoto wa DJ maarufu nchini Marekani anayefahamika kama DJ Khaled ambaye katika ukurasa wake wa Instagram ndiyo kwanza juzikati amegonga followers milioni 2. Tangu akiwa mtoto Baba yake ‘kasha-mbrand’ kwa kufanya naye kazi mbalimbali za muziki, huku Asahd akiwa kama prodyuza msaidizi wa lebo yake ya ‘We the Best’ hali iliyofanya watu wengi wamfuatilie na kuzidi kufahamika zaidi duniani kote.
NORTH WEST
Ni mtoto wa mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian na Rapa Kanye West ambaye kwenye ukurasa wake wa Instagram anatumia jina la Norisblackbook akiwa na followers 369,000. Akaunti ya mtoto huyu nadhani haiendeshi katika ‘userious’ unaotakiwa ndio maana ana mashabiki wachache sana tofauti na wazazi wake wenye mamilioni ya followers.
ROYALTY BROWN
Ni mtoto wa staa wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown ambaye katika ukurasa wake wa Instagram anatumia jina la Missroyaltybrown akiwa na followers 209,000.
BLUE IVY CARTER
Ni mtoto wa wanamuziki maarufu nchini Marekani, Beyonce na Jay Z ambaye katika ukurasa wake wa Instagram ana followers 145,000. Huenda ndio akawa mtoto wa staa mwenye followers wachache zaidi kuliko wote na yote ni kwa sababu wazazi wake hawaweka umakini zaidi katika kum-brand mtoto wao katika mitandao na ndio maana mara nyingi huwa wanamposti katika akaunti zao na sio katika akaunti yake
Makala: Shamuma Awadhi