JAMII ya Kabila la Wamwera waishio jijini Dar es Salaam wamefunika kwa kuonyesha utamaduni wao wa asili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Utamaduni wa Mtanzania yaliyofanyika leo Jumamosi, Oktoba 27, 2018 katika Kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama jijini Dar.

Katika maadhimisho hayo, Wamwera ambao asiliyao ni Mkoa wa Lindi walipata fursa ya kuonyesha michezo yao ya ngoma hasa ngoma yao ya Litono ambayo iliwavutia watu wengi na kuonekana wakishangilia na kuicheza.

Mbali na Litono, Wamwera wameonyesha vitu vyao vya asili vikiwemo viti, mikeka, mavazi, vitanda, vinyago na vingine vingi.

Wanawake wa Kimwera walionekana kulisakata vyema rumba wakiungana na vijana wa kabila hilo jambo ambalo limevuta hisia na kuamsha furaha miongozni mwa waliohudhuria.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS