The House of Favourite Newspapers

Mtanzania Apigwa Urusi, Amwaga Machozi

BAADA ya hivi karibuni bondia Hassan Mwakinyo kufanya kweli kwenye pambano lake nchini Uingereza, juzi Jumamosi ilikuwa siku mbaya baada ya Mtanzania Mfaume Mfaume kuchakazwa kwenye pambano lake dhidi ya Mrusi Vaghinak Tamrazyan la kuwania ubingwa wa dunia kilo 66.5 lililopigwa nchini Urusi. Mfaume alipoteza pambano hilo kwa TKO katika raundi ya pili baada ya kuanguka katika raundi ya pili ambapo alihesabiwa na mwamuzi wa pambano hilo hadi saba, kisha mwamuzi akamaliza pambano hilo akiashiria Mfaume amepoteza.

Akizungumza na Championi Jumatatu, promota Jay Msangi ambaye alienda na bondia huyo, amesema kupoteza pambano kwa bondia huyo kuliwashangaza watazamaji wengi ambao walihudhuria pambano hilo kutokana na Mfaume kuinuka na kuwa sawa baada ya kuanguka lakini mwamuzi huyo akamaliza pambano hilo na Vaghinak kutangazwa bingwa.

“Refarii alimhesabia na Mfaume akainuka ilipofika saba akiwa tayari kuendelea na mpambano na akiwa katika hali nzuri bila madhara yoyote, kwa mshtuko refarii aliamua kumaliza pambano. “Jambo hilo liliwashtua wadau wote ukumbini hata kumuacha bondia Mfaume akilia juu ya ulingo kwa machungu akiwa haelewi kwa nini refarii kamaliza pambano mapema. Mfaume amepigwa TKO ya raundi ya pili, hivyo mpinzani wake Vaghinak wa Urusi kupewa ubingwa,” alisema Msangi.

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.