MKE wa aliyekuwa Habari wa Kituo cha Runinga cha Star Tv na Radio Free Africa, (Sahara Media Group) ambaye pia alikuwa mkongwe kwenye tasnia hiyo, Samadu Hassan, Bi. Anna Kabase amefunguka juu ya kifo cha mumewe ka kusema huenda kilisababishwa na ‘presure’ kushuka.
Mjane huyo amesema hayo leo Novemba 1, 2018 wakati akizungumza na Global Digital na kubainisha kwamba mumewe alifariki jana usiku, nyumbani kwake eneo la Miembe Mitatu, Nyamagana jijini Mwanza, majira ya saa tano na mwili wake kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kuhifadhiwa hadi ndugu zake kutoka Dar es Salaam na Dodoma watakapofika kwa ajili ya kuandaa taratibu za kusafirisha kuelekea nyumbani kwao Bukoba hapo kesho kwa mazishi.
Bi. Anna amesema; “Huenda chanzo cha kifo chake kimetokana na taarifa ya mtoto wake aliyompa ya kudaiwa fedha za chuoni ambazo zilikuwa zikihitajika lakini yeye kwa wakati huo hakuna fedha hizo jambo alilolieleza kwamba linaweza kuwa limechangia kwa kiasi kikubwa kifo hicho,” .
“Alipopigiwa simu na wanaye walizungumza, lakini alipomaliza mazungumzo ndipo akaomba maji ya kunywa na hatimaye akaishiwa nguvu na baadaye akapoteza fahamu na kufariki dunia.
“Kwa kweli namwombea kwa Mungu marehemu mme wangu awekwe mahali pema peponi, Amina,” alimalizia.
PICHA NA DENIS MTIMA | GPL
Comments are closed.