×

TCU Yafuta Usajili wa Chuo Kikuu, Yaamuru Wanafunzi Wahamishwe – Video

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefuta usajili wa kituo cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishiwe katika Kampasi Kuu ya chuo hicho iliyopo Masoka, Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 9, 2018 Katibu Mtendaji wa TCU), Prof. Kihampa amesema TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya na kuamuru kuhamishwa mara moja wanafunzi wa shahada ya kwanza wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2018/19 katika programu tisa za shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vinne ambapo ni;

 

Wanafunzi wote wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) – Dar es Salaam, Programu ya Shahada ya Tiba na Upasuaji, Shahada ya Sayansi na Uuguzi.

 

Wanafunzi wote wanaosoma Programu ya Udaktari wa Bbinadamu, Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu James (Ajuco), Songea- Ruvuma, Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) Moshi, Kilimanjaro, za shahada ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma na Sanaa na Utawala.

 

Amefafanua pia imezuia udahili kwa wanafunzi wanaosoma Programu za Shahada ya Elimu na Mahitaji Maalumu (Arts), Shahada ya Elimu na Mahitaji Maalumu (Sayansi), Shahada ya Sayansi na Elimu na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastiano Kolowa (SEKOMU), Lushoto-Tanga.

TCU Yafanya Maamuzi Magumu/ Vyuo Viilivyofutiwa Usajili Hivi Hapa