×

SAMIA, MGHWIRA WAUAGA MWILI WA ANNA MENGI – VIDEO

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, ameungana na waombolezaji katika ibada ya kuuaga mwili Mercy Anna Mengi,  katika kanisa la Dayosisi ya Kaskazini – Usharika wa Moshi Mjini (KKKT), leo Jumamosi, Novemba 10, 2018.

Samia aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, wabunge, viongozi wa dini katika kuaga mwili huo ambao umepelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya mazishi.

Aidha, viongozi hao wamepata pia fursa ya kumpa pole, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi, familia na watoto wa marehemu.

Bi. Mercy ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa IPP Media, alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hosptali ya Mediclinic Morningside ya Johannesburg nchini Afrika Kusini Oktoba 31 mwaka huu.

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HAPA