The House of Favourite Newspapers

Aliyewasafirisha Watekaji wa Mo Dewji, Asimulia A-Z Ilivyokuwa!! – Video

Nyumba inamodaiwa kufichwa Mohamed Dewji mara baada ya kutekwa Okotoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colosseum imegundulika na imeoneshwa leo na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

 

Dereva Taxi aitwae TWALIB MUSSA ambaye hupaki Taxi yake maeneo ya White Sand Hotel, baada ya kukamatwa na kuhojiwa amekiri kuwabeba watuhumiwa hao na kuwasaidia kwa moja ama nyingine kufanikisha kumteka Mohammed Dewji na kumficha kwa siku tisa.

 

“Mimi huwa ninapaki pale White Sand Hote, tunapakia kwa zamu, hivyo zamu yangu ilivyofika niliitwa na watu wa reception wakaniambia kuna wageni, nilikuna nao na kuzungumza nao walikuwa wanahitaji nyumba ya kupanga, nilimtafuta dalali aitwaye Mohammed ndiye alinionyesha hii nyumba iliyopo Mbezi Beach, Mtaa wa Mwansasu jijini Dar es Salaam,” alisema Twalib.

 

Dereva huyo anaendelea kusema kuwa nyumba hiyo alipanga yeye kwa niaba ya watekaji hao wanaodaiwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini, kwa gharama ya dola 1,300 kwa mwezi kwa muda wa miezi sita.

 

Imeelezwa pia kwamba, Oktoba 20 baada ya kumuachia na kumtelekeza katika viwanja vya Gymkhana, vilivyopo maeneo ya Posta, dereva huyo aliwachukua na kuwapeleka katika Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani, Ubungo ambako walipanda basi na kuondoka.

 

VIDEO: MSIKIE MTUHUMIWA HUYU AKIFUNGUKA

Comments are closed.