×

MTANZANIA AWEKA REKODI, ASHINDA URAIS CHUO KIKUU URUSI

UMOJA WA WANAFUNZI NA VIJANA WA KIAFRIKA CHUO KIKUU CHA URAFIKI CHA URUSI (PEOPLES’ FRIENDSHIP UNIVERSITY OF RUSSIA) AU PATRICE LUMUMBA UNIVERSITY.(ASSAFSTU-RUDN) WAKAMILISHA UCHAGUZI MKUU

KUHUSU CHUO CHA PATRICE LUMUMBA
-Chuo Kikuu cha Urafiki cha Watu wa Urusi au Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba Kilianzishwa mwaka 1960 na kwanza kikapewa jina la Patrice Lumumba University kuanzia 1961-1992.
-Chuo hiki kina mataifa zaidi ya 155 na tamaduni za watu wote duniani na ustaarabu wa dunia na dini zote na kina walimu na wahadhiri na maprofesa kutoka nchi mbalimbali duniani lakini zaidi ni Warusi wenyewe.

KUHUSU UCHAGUZI
-Nafasi ya Uraisi wa Wanafunzi na Vijana wote wa Kiafrika Chuo cha Patrice Lumumba inagombewa kila mwaka na mgombea hawezi kurudia kugombea tena. Ni mara moja tu kwa mwaka !
-Mtanzania Mohamed Mansour Nassor ambae ni Mhadhiri Msaidizi katika Chuo cha Patrice Lumumba katika Kitivo cha Uchumi, idara ya Jiografia na Uchumi wa Kikanda (Department of Geography and Regional Economy) na Pia ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Uchumi(PhD in Economics) katika idara ya Siasa ya Uchumi (Dapartment of Political Economy). Yeye ndio mwaka huu wa 2018/2019 kama Mtanzania anashika nafasi hii kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki mwaka 1960.

-Ndugu Nassor Mohamed Mansour amechukua nafasi hio ya Urasi baada ya kumaliza muda wake Raisi aliepita kutoka Madagascar, Mwanadada Alice Lafara.
-Nchi zilizopiga kura kumchagua Raisi Mohamed Mansour Nassor zilikua ni 45 kupitia Wawakilishi na Maraisi wa Wanafunzi wa nchi hizo.

-Inasemekana kuwa Wagombea wa Uraisi walikua ni wa 3 lakini karibu kufikia siku ya Uchaguzi inasemekana walitolewa kwa sababu tofauti kama kutokidhi vigezo kwa Mmoja kutoka Nigeria.
-Ndugu Mohamed alibakia peke yake kwa kukidhi vigezo na sifa alipigiwa kura za NDIO au HAPANA alishinda kwa kura 23 kati ya 25 za NDIO.
-Taarifa zinaeleza kuwa Raisi mteule, Mohamed Nassor alikuwa na sifa nyingi na muhimu za kunyakua nafasi hio(TIZAMA CV).

-Kwa Afrika Mashariki Ndugu Mansour anakua ndio kijana wa Pili kutoka Afrika Mashariki kushika nafasi hio baada ya miaka ya nyuma Mwanadada kutoka Kenya , Lilian kushika nafasi hio. Nafasi hii imekua ikishikwa sana na vijana wa Kiafrika kutoka Afrika ya Maghribi hasa Nigeria.
-Umuhimu wa nafasi hii ya Uraisi ni kuwa kwanza Raisi anaingia katika washauri wa Mkuu wa Chuo kwa Wanafunzi wa Kiafrika.

-Piakupitia na kusaidia na jopo la wasadizi wake Raisi anaweza kufanya ziara kutembelea mabalozi wa Kiafrika wanaowakilisha nchi zao nchini Urusi kwa lengo la kufanya mazungumzo yenye tija ya kusaidia Wanafunzi wa Kiafrika Chuoni hapo na kupeperusha bendera za nchi za Afrika juu zaidi kimataifa hasa nchini Urusi, anaweza kushughulikia changamoto na matatizo ya wanafunzi wa Kiafrika katika maendeleo ya ufuatiliaji masomo endapo yatajitokeza, matatizo mengine nje ya Chuo yasio ya makusudi yanayomkuta Mwanafunzi wa Kiafrika, kusimamia na kufuatilia Maslahi ya Wanafunzi wa Kiafrika Chuoni hapo, kuandaa mikutano mbalimbali ya Kimataifa yani International Conferences na mabalozi wa Nchi za Afrika waliopo Urusi, kuandaa wiki ya Utamaduni wa MWAFRIKA Chuoni hapo nk.

 

-Raisi mteule Mtanzania, Mheshimiwa Mohamed Mansour Nassor atakua na jopo la wasaidizi wake kutoka nchi tofauti za Afrika waliochaguliwa pamoja nae yani Makamu wa Raisi Ndugu Mahamat Muqaddam kutoka Chad, Katibu Mkuu, Diouf Daur kutoka Senegal na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Ndugu Dju Orlindo kutoka Guinea Bissau.

 

Pia kuna Makatibu na Manaibu Katibu wa idara mbalimbali kama Idara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Fedha na Uchumi, Elimu nk.
-Kwa hakika hii ni heshima kubwa kwa Taifa la Tanzania na sifa njema na Taifa limetangazwa vyema sana kwa kijana wa Kitanzania kushika nafasi hii kubwa katika moja ya Chuo Kikubwa kama hiki cha Kimataifa cha Patrice Lumumba.

Mungu ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!

TAWASIFU (CV) NA HISTORIA YA KIJANA WA KITANZANIA ALIESHINDA KWA MARA YA KWANZA UCHAGUZI WA NAFASI YA URAISI WA WANAFUNZI NA VIJANA WA KIAFRIKA KATIKA CHUO KIKUU CHA PATRICE LUMUMBA(PFUR)MJINI MOSCOW,URUSI TANGU KUANZISHWA KWAKE CHUO HIKO 1960

TAARIFA BINAFSI
Jina Kamili: MOHAMED MANSOUR NASSOR
-Mahali pa Kuzaliwa:Zanzibar
-Tarehe ya Kuzaliwa:30/06/1987

ELIMU
-2016-Mpaka sasa: Shahada ya Uzamivu katika Uchumi(PhD in Economics), Idara ya Siasa ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba
-2017-Mpaka sasa-Shahada ya Uzamivu ya Usuluhushi wa Migogoro na amani(Conflict Resolution and Peace Building),Idara ya Masomo ya Mtandaoni,Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU)
-2016/2017-Astashahada ya Uzamili ya daraja la Kwanza ya Usimamizi wa Mahusiano ya Kigeni(First Class Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations), Chuo cha Diplomasia cha Tanzania(CFR)
-2014-2016-Shahada ya Uzamili ya daraja la Kwanza ya Usimamizi wa Kimataifa(First Class Masters Degree in International Management, Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba, Moscow,Urusi
-2010-2014-Shahada ya Kwanza ya Uchumi(Bachelor Degree in Economics)- Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba, Moscow Urusi
-2010-2014-Shahada ya Lugha ya Kirusi, Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba,Moscow,Urusi
-2006-2008-Elimu ya Kidato cha Sita(Form six)Shule ya Sekondari Tambaza,Dar es Salaam
-2002-2005-Elimu ya Kidato cha Nne(form four),Nur Islamic Seminary),Dar es Salaam
-1995-2001-Elimu ya Shule ya Msingi, Dar es Salaam

MAFUNZO MAFUPI
1-Mafunzo ya Diplomasia ya Uchumi(Economic Diplomacy)
2-Mafunzo ya Diplomasia na Itifaki za Kidiplomasia(Essentials of Diplomacy and Protocol)
3-Mafunzo ya Uongozi wa jamii(Community Leadership)
4-Mafunzo ya Kompyuta(Basic Computer Program Training)
5-Mafunzo ya Vitedo-Ubalozi wa Yemen nchini Urusi

UJUZI WA LUGHA
1-Kiswahili
2-Kiingereza
3-Kirusi
4-Kiarabu
5-Kifaransa
6-Kihispani
7-Kireno

KAZI
-2017-Mpaka sasa:Mhadhiri Msaidizi katika Uchumi, Idara ya Jiografia na Uchumi wa Kikanda,Kitivo cha Uchumi ,Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba
-Mchambuzi wa Masuala ya Siasa,Diplomasia,Mahusiano ya Kimataifa na Uchumi katika Redio na Televisheni vyombo za Tanzania na za Kimataifa(BBC,DW,IRIB)
-Mwandishi wa Makala(zaidi ya 30 kwa sasa) katika magazeti ya Tanzania, Majarida ya Kimataifa nchini Urusi na Ulaya Magharibi katika masuala ya Siasa,Diplomasia,Mahusiano ya Kimataifa na Uchumi.

UZOEFU WA UONGOZI TANZANIA
2018-Mpaka sasa: Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Kata ya Ruvu , Wilaya Kibaha Vijijini
2017-Mpaka sasa: Mwenyekiti wa Tawi la UVCCM Kata ya Ruvu Wilaya ya Kibaha Vijijini
2016/2017: Kiongozi wa Darasa la PGD-MFR,Chuo cha Diplomasia,Dar es Salaam
2016/2017: Mbunge wa Serikali ya Wanafunzi, Chuo cha Diplomasia cha Tanzania

UZOEFU WA KIMATAIFA NA UONGOZI URUSI
2014-Mpaka sasa: Kushiriki na kuwasilisha mada kuhusu Afrika, Tanzania , Uchumi na Diplomasia katika mikutano ya Kimataifa
2018-Mpaka sasa: Balozi wa Chama cha Watanzania waliowahi kusoma nchini Urusi(SOYUZ Alumni Association of Tanzania)
2018-Mpaka sasa: Makamu Mwenyekiti wa Diaspora ya Watanzania nchini Urusi
2017-Mpaka sasa: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kiswahili cha Moscow (CHAKIMO)
2017/2018: Waziri Mkuu wa Wanafunzi wa Kitanzania Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba, Moscow
2012-2013: Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo wa Umoja wa Wanafunzi wa Kitanzania Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba,Moscow
2013-Mpaka sasa: Mlezi wa Tawi la CCM la Patrice Lumumba,Moscow.

TUZO
2004: Mwanafunzi bora kwa Kidato cha tatu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika masomo ya Kiingereza, Fizikia,Maarifa ya Uislam
2005: Mwanafunzi bora wa Shule ya Sekondari ya Nur Islamic kwa miaka 2002-2005
2016: Mwanafunzi bora katika Kitivo cha Uchumi kwa vijana wa Kiafrika katika Shahda ya Uzamili
2017: Mwanafunzi bora kwa Astashahada Uzamili ya Usimamizi waMahusiano ya Kigeni(Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations), Chuo cha Diplomasia cha Tanzania
2018: Mwanafunzi bora Tanzania kupitia TAHLISO (Tanzania Higher Learning Institution Student Organization) katika kiwango cha Astashahada ya Uzamili(Post Graduate Diploma)

NAFASI ALIZOGOMBEA CCM
2017-Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam
2017-Mwenyekiti wa CCM Kata ya Jangwani, Wilaya ya Ilala,Dar es Salaam
2017-Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA).