×

OFISA MALAZI (UDSM) AKABIDHIWA  NDINGA YAKE NA TBL

Meneja  Udhamini na Mawasiliano ya Wateja TBL, David Tarimo (kulia) akimkabidhi ufungua wa gari, Julitha Kilawe, ambaye ni mshindi wa promosheni.
David Tarimo (kulia) akimkabidhi kadi ya gari, Julitha Kilawe.
 Julitha Kilawe akiwa ndani ya gari lake.

 

 

 

KAMPUNI ya TBL leo imemkabidhi mshindi wa kwanza wa zawadi kubwa ya gari  aina ya Renault KWDI, Julitha Kilawe, ambaye ni Ofisa Malazi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa droo ya promosheni inayojulikana kama ‘TBL Kumenoga”.

 

TBL ilizindua promosheni hiyo inayojulikana kama ‘TBL kumenoga,Tukutane baa’ kwa lengo la kuwashukuru wateja wake na inafanyika kwenye baa mbalimbali nchini  ambapo washiriki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWDI kwa kila mshindi wa droo kubwa ya mwezi na promoheni itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia ilipozinduliwa mwezi uliopita.

 

Meneja  Udhamini na Mawasiliano ya Wateja TBL, David Tarimo, amesema promosheni hiyo itafanyika kupitia chapa maarufu za bia zinazozalishwa na kampuni ambazo ni Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

 

Kwa upande wake,Julitha Kilawe, ambaye ni mshindi katika promosheni hiyo amepongeza Kampuni ya TBL kwa kuendesha shindano hilo kwani hakutegemea kama angeliweza kujishindia gari hiyo kwani katika maisha yake alikuwa hajawahi kumiliki gari.

 

Vilevile mbali na zawadi kubwa ya gari zipo zawadi nyingi za kujishindia kupitia promosheni hiyo ikiwemo bia za bure na kwamba  promosheni hiyo itakuwa inafanyika wikiendi ambapo kila sehemu ya promosheni kutakuwepo bendera ya TBL Kumenoga.

 

Alisema ili kushiriki promosheni hiyo ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ anachotakiwa kufanya mteja ni kununua bia tatu za chapa zilizopo kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba ambazo wanapaswa kuzituma kupitia simu zao za mkononi kwenda namba 15451 kwa kutumia mitandao ya simu ya makampuni ya Vodacom, Tigo na Airtel.Wateja wenye mitandao mingine ya simu wanaweza kushiriki promosheni kupitia tovuti ya http://www.tblkumenoga.co.t