
BENKI ya NMB imetoa vifaa vya michezo kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya mashindano ya majeshi yanayotarajia kufanyika Aprili, mwakani.
Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na Kati wa NMB, Salie Mlay amesema vifaa walivyokabidhi kwa JWTZ vina thamani Sh milioni 12.5.
“Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu mbalimbali za JWTZ kwa michezo ya soka, netiboli na kikapu ambavyo thamani yake ni Sh milioni 12.5. Timu hizo zinatarajiwa kushiriki mashindano ya majeshi ambayo yatafanyika mwakani,” alisema Mlay. 