×

DIAMOND KUKINUKISHA UPYA WASAFI FESTIVAL IRINGA

Rais wa Crew ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akifanya yake.

 

RAIS wa Crew ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, baada ya kukinukisha vilivyo kwenye uzinduzi wa Wasafi Festival katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wikiendi iliyopita, amesema kuwa Ijumaa hii ya Novemba 30, moto unaenda kuwaka katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.

 

Akizungumza Diamond alisema kuwa baada ya uzinduzi huo, sasa nguvu inahamia Iringa kwenye Uwanja wa Samora ambako wasanii wengine wapya wameongezeka kwa ajili ya kunogesha burudani hizo sambamba na wasanii wote wanaounda lebo ya WCB.

“Novemba 30 tunaenda sasa kuanza safari ya makamuzi yetu ikiwa ni siku kadhaa tu baada ya kuzindua Festival yetu pale Mtwara, naomba mashabiki wote wa burudani waje kuona ni namna gani wasanii wetu wamejipanga.

“Mapinduzi ya burudani yataendelea zaidi kutokea siku ya Jumapili ya Desemba 2 mwaka huu ambapo tutakuwa tukiumiza nyasi za Uwanja wa Jamhuri pale mjini Morogoro, kwani pale pia tunatarajia kuongeza wasanii huku tukipunguza ambao watakuwa na siku chache tu wametumbuiza pale,” alisema Diamond.