Zitto Kabwe Aungana na Chadema Rufaa Ya Mbowe (Picha+Video)
Global Publishers November 28, 2018
SHARE THIS:
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakisalimia baada ya kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
MBUNGE wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wameshawasili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Jumatano kusikiliza rufaa ya dhamana yao iliyofutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23.
Kiongoziwa chama cha ACT–Wazalendo Mhe. ZittoKabwe amefika katika mahakama hiyo akiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji.
Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji (katikati) akiongea jambo na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.Viongozi mbalimbali wa upinzani wakiendelea kujadili mambo mbalimbali. Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye (kulia) akiongea jambo.