14 Waliofariki Kwa Ajali Ya Gari Tarime Wazikwa – Video
MAZIKO ya pamoja ya watu 14 waliofariki katika ajali Jumanne Novemba 27, 2018 baada ya magari mawili ya abiria aina ya Hiace kugongana katika eneo la Komaswa maarufu kama Kwa-Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara ambapo magari mawili ya abiria aina ya Toyota Hiace yaligongana uso kwa uso na kuteketea kwa moto, yamefanyika leo katika eneo waliopata ajali na wengine wawili wamechukuliwa na ndugu zao.
Maziko hayo yamehudhuriwa na Waziri Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine mbalimbali.
Katika maziko hayo Waziri Lugola ametoa onyo kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani kwa kuwa serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha wanadhibiti ajali kwa kutoa leseni kwa madereva waliosoma na kufaulu vizuri pia kuwepo kwa adhabu kali kwa madereva wazembe.
Vilevile, Ummy Mwalimu amesema serikali itawahudumia majeruhi wote kwa kutoa gharama za matibabu mpaka watakapopona.
PICHA: IDDY MUMBA/TARIME -GPL
Comments are closed.