AUTOPRO YAWAPELEKA BEACH YATIMA WA ‘GREEN PASTURES’ DAR
Global Publishers November 29, 2018
SHARE THIS:
Picha ya pamoja ya watoto yatima wa Kituo cha ‘Green Pastures’ cha Mapinga jijini Dar es Salaam na wadau wengine wa Kampuni ya Autopro mara baada ya kuwasili eneo la Kunduchi Beach kujumuika katika michezo na watoto hao.Baadhi ya watoto yatima wakimsikiliza Meneja Ufundi wa Autopro, Willbard Gandu (wa kwanza kulia) alipokuwa akizungumza na watoto hao. Watoto yatima wa Kituo cha ‘Green Pastures’ cha Mapinga wakipata chakula Kunduchi Beach mara baada ya michezo mbalimbali ya watoto.Muonekano wa ofisi za Autopro zinazotoa huduma za ‘Car service, tires, diagnosis, 3D wheel alignmnent balance, accessories, brakes, suspension, batteries, bushes, autodetailing iliyopo eneo la Goba Mwisho, Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Autopro imejumuika na watoto yatima wa Kituo cha ‘Green Pastures’ cha Mapinga jijini Dar es Salaam ikiwa ni tukio la kurejesha sehemu ya faida yake kwa wahitaji. Katika tukio hilo kampuni ya Autopro inayotoa huduma za ‘Car service, tires, diagnosis, 3D wheel alignmnent na balance, accessories, brakes, suspension, batteries, bushes, autodetailing eneo la Goba mwisho jirani na Banki ya CRDB iliwapeleka Kunduchi Beach watoto wa kituo hicho pamoja na kujumuika katika chakula cha mchana.
Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Ufundi wa Autopro, Willbard Gandu alisema waliamua kujumuika na watoto hao kwa pamoja na familia zao ili kuwafariji jambo ambalo ni jema katika jamii.