The House of Favourite Newspapers

SISTER FAY AFUNGUKA ANAVYOHENYESHWA NA TCRA

Faidha Omary ‘Sister Fay’

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Faidha Omary ‘Sister Fay’ ameeleza anavyohenyeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kisa kujiachia mitandaoni.  

 

Akichonga na Za Motomoto News, Sister Fay alisema tangu walipokamatwa na polisi na mumewe Holy Star mwezi wa tisa kutokana na kutumia mtandao vibaya kwa video zao tata, wamekuwa wakihenyeka na hawapo mtandaoni kutokana na simu waliyokuwa wanaitumia kushikiliwa polisi mpaka sasa.

 

“Tuliingia matatani kwa sababu ya video na picha tulizokuwa tunawekakwenye Mitandao na tukaamuriwa kuacha simu zetu pamoja na laini kule polisi huku tukipigwa marufuku kutumia mitandao mpaka tutakaporuhusiwa na TCRA kwa hiyo ndiyo maana tupo kimya,” alisema Sister Fay.

Stori: Shamuma Awadhi

Comments are closed.