The House of Favourite Newspapers

TANGA: Basi Laua Waawili na Kujeruhi 21

WATU wawili wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa huku sita kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la Royal Classic waliokuwa wakisafiria, kuacha njia na kupinduka eneo la Kibaoni wilayani Lushoto jana Jumanne Desemba 11.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema basi hilo lilikua likisafiri kutoka Tanga kwenda wilayani Lushoto. Amedai chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.

 

“Majeruhi sita kati ya 21 hali zao ni mbaya na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa matibabu zaidi,” amesema Bukombe.

DC SABAYA na MURO Wawasha Moto Wananchi Kupigwa Risasi!

Comments are closed.