MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, imemhukumu mwanamke, raia wa Msumbiji, Ana Moisie Chissano, kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kilogramu 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.
Mshtakiwa amefungwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.
Hukumu hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Jaji Lilian Mashaka baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka hayo na kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.
Aidha mahakama imeamuru dawa hizo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.
Chanzo stori: Michuzi Blog
Comments are closed.