×

Maua Sama, Roma, Mr Blue, Weusi Wafunika Fiesta Dar (Picha +Video)

Kundi la muziki likiimba wimbo wa Vibe Kama Loooote kwenye jukwaa la Fiesta Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar.

WAPENZI wa burudani usiku wa kuamkia leo wamepata burudani ya aina yake katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar wakati Tamasha la Fiesta lililosheheni mastaa kibao lilitoa burudani ya kufa mtu.

Msanii Maua Sama (kulia) na wacheza shoo wake wakitoa burudani.

Awali tamasha hili lilitarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders, Dar,  lakini lilisitishwa kutokana na sababu mbalimbali.

Wasanii wa Kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Nikki 2 (kulia), G-Nako (kushoto) wakifanya shoo.

Mastaa waliopanda kwenye jukwaani  ni  AliKiba na kundi lake,  Kundi la Nako 2 Nako likiongozwa na Joh Makini na wenzake, Juma Nature, Fid Q, Chege, Mr Blue, TID, Vanessa Mdee, Rich Mavoko, Msami, Maua Sama, The Mafik, Christian Bella, Rosa Ree na wengine wengi.

Mr Blue akifanya yake akiwa na Chid Benz.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanaounda kundi la Rostam —  Roma (katikati) na Stamina pamoja Maua Sama — wakifanya yao.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL

Huyu MSAMI Sasa BASI! Afanya kufuru Stejini, FIESTA!

Cheki ROSTAM, MAUA SAMA Walivyo iokota FIESTA!