The House of Favourite Newspapers

CHEMICAL ABEBA JINA LA KONKI

Claudia Lubao ‘Chemical’

MWANADADA anayefanya Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’ amelikubali jina la Konki baada ya kuwa msanii wa kwanza kutoa shoo kwa saa moja bila kutetereka akiwa stejini huku akitaka kuongezewa muda.

 

Chemical alifanya hivyo kwenye Tamasha la Fiesta lilifanyika wikiendi iliyopita kwenye Viwanja wa Posta
jijini Dar.

Ijumaa ilipotaka kujua siri ya yeye kufanya hivyo, Chemical alisema kuwa siri kubwa ni kutokana na maandalizi anayoyafanya kama msanii ambaye anatakiwa akipanda stejini awapatie mashabiki wake shoo wanayotarajia.

 

“Ninachofanya ni maandalizi zaidi hasa ya kutengeneza sauti na kumiliki steji ili kuweza kuwapa mashabiki wangu kile kitu ambacho wanahitaji kutoka kwangu,” alisema Chemical aliyefunika baada ya kupanda stejini na kukubali jina la Konki alilopewa na mashabiki wake.

Comments are closed.