Katika kuhakikisha wanatoa shukrani kwa wateja wao kwa kipindi chote walichoshirikiana nao, Kampuni ya mtandao wa simu ya Halotel wamefanya tamasha La Asante Halotel katika uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.
Katika tamasha hilo ambalo Halotel wametoa misaada kwa wasiojiweza na zawadi kwa wateja wao, limeambatana pia na burudani kabambe kutoka kwa wasanii wa nyumbani akiwemo Gigy Money.