×

GLOBAL HABARI JAN 10: WAITARA ANG’AKA, AWAONYA VIKALI WAMILIKI WA SHULE – VIDEO

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwita Waitara, ametoa onyo kwa wamiliki wa shule binafsi wanaowarudisha wanafunzi nyumbani kwa kukosa ada baada ya kupandisha ada ghafla bila ya kuwataarifu wazazi.

Naibu Waziri Waitara amesema kitendo cha kumrudisha mwanafunzi nyumbani kinamvuruga na kumvunja moyo wa kusoma tena na kutoa agizo kwa wamiliki wote wa shule binafsi kuwasiliana na wazazi kuhusu ada na sio kukurupuka na kuwarudisha nyumbani.

Pia Waitara amesema kuwa serikali imetoa siku tisini kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao watakuwa bado hawajaripoti shuleni na baada ya hapo nafasi zao zitakuwa zimefutwa.

Pia waitara amesema kuwa serikali imejipanga kuziwajibishwa shule zote zilizopanga wastani wao binafsi tofauti na wastani elekezi wa serikali hali inayopelekea kuwarudisha wanafunzi nyumbani.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club