MWILI wa mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana umekutwa ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kutupwa kando ya barabara katika eneo la Karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii mkabala na Ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Global TV Online imefunga safari mpaka eneo la tukio na hii ndiyo hali halisi ilivyokuwa baada ya kuukuta mwili huo huku wananchi wa eneo hilo wakihamaki kutokana na tukio hilo la kinyama.
Mjumbe wa mtaa huo Bi Fortunata Mshindo amesema jana mchana yeye na wananchi wengine walipita katika eneo hilo na hakukua na kitu chochote huku pia akisisitizia uongozi wa manispaa kuweka taa katika eneo hilo ili kupunguza matukio ya kihalifu.
Maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio wakauchukua mwili huo kwa uchunguzi zaidi.