Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Leo January 23, 2019, amekutana na viongozi mbalimbali wa Dini Ikulu Dar es Salaam na kuongea nao.
“Pale Hospitali ya Bugando Mwanza kulikuwa na mtatizo mengi, asilimia kubwa ya mishahara inalipiwa na Serikali, lakini kuna wizi wa ajabu pale, ipo skendo ya fedha, Mtawa aliamua kujiua, juzi wamekuta amefungua akaunti nyingine ya Tsh 100m ambayo walikuwa hawaijui.
“Nampongeza Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), (Askofu Gervas John Nyaisonga) ameenda na kushughulikia tatizo la Bugando, sitaki kuwakwaza viongozi wa dini, nataka maombi yenu yawe ni ya kuniombea ili mabaya yenu nisiyaseme.
“Ndani ya Serikali yangu matatizo ya viongozi wa dini lazima yatatuliwe, kutatua matatizo haya hutatui tatizo la mtu mmoja, bali unatatua matatizo ya watu wengi, wakati mwingine tunajipa laana sisi wenyewe tu.
“Ndiyo maana huwa ninawasihi kila siku viongozi wa dini, endeleeni kuniombea nisije nikapata kiburi, nitafanya kazi kama Mtumishi na sio Mtawala. Uongozi mara nyingi unawapa watu kiburi wanafikiri wao ndio wao,” amesema Rais Magufuli.
