×

MPOTO AMEBAKI NA SAUTI YA OLIVER MTUKUDZI – VIDEO

Msanii wa nyimbo za asili nchini, Mrisho Mpoto, amebaki na sauti ya Mwanamuziki nguli nchini Nigeria, Oliver Mtukudzi ambaye amefariki siku mbili zilizopita huku akiacha simanzi kwa watu wote duniani na waliomfahamu na kupenda nyimbo zake hususani ile ya ‘Neria’ ambayo ndiyo iliyompa umaarufu mkubwa.

Akizungumza na Global TV mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi la ‘SIZONJE’ lililopo chini ya Mrisho Mpoto, Ismail, amesema kabla ya kifo cha Nguli huyo walishafanya nae kazi na kilichokuwa kimebakia ni kushuti nae video tu, kitu ambacho kitabaki kuwa historia kwa nguli huyo ameshamaliza muda wake hapa duniani.