Rais Samia Afanya Ziara Ujenzi Daraja La Tanzanite Dar – ( Picha +Video)
Global Publishers November 4, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Tanzanite linaloendelea kujengwa katika eneo la Selander Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021. Kulia ni mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatius Mativila.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatius Mativila kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Tanzanite linaloendelea kujengwa katika eneo la Selander Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021.
Rais Samia Suluhu Hassan muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea Glasgow, Scotland leo Novemba 4, 2021 amefanya Ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Tanzanite ambalo ujenzi wake umefikia 97.6% kukamilika